Jumamosi 19 Aprili 2025 - 07:19
"Inatumika kwenye nchi zote isipokuwa Israel"

Kuna kanuni isiyoandikwa miongoni mwa serikali za nchi nyingi za Kiislamu - kwamba mambo yanapoharibika nyumbani, zigeuze lawama kuelekea kwa Taifa la Israel.

Shirika la Habari la Hawza - wiki iliyopita mamlaka ya jiji la Dhaka, mji mkuu wa Bangladesh, ilitangaza kuwa itarudisha tamko "Inatumika kwa nchi zote isipokuwa Israel" kwenye pasipoti zinazotolewa kwa raia wake. Tamko hili ambalo liliondolewa mwaka 2021 na serikali ya waziri mkuu wa zamani Sheikh Hasina, hata hivyo halikufuatiliwa kwa juhudi zozote za kidiplomasia za kujihusisha na Israel, wala kutambua utawala wa Kizayuni.

“Kwa miaka mingi, pasipoti zetu zilikuwa na kipengele cha ‘isipokuwa Israel’. Lakini serikali iliyopita ghafla ilikiondoa,” alisema Brigedia Jenerali Mohammad Nurus Salam, mkurugenzi wa hati za kusafiria katika Idara ya Uhamiaji, na akaongeza: “Tulikuwa tumezoea kuona maneno ‘isipokuwa Israel’ yameandikwa kwenye pasipoti zetu. Sijui kwa nini waliyaondoa. Ukizungumza na watu nchini kote, utaona wanahitajia mstari huo urudi kwenye hati zao za kusafiria. Hakukuwa na haja ya kuuondoa.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha